KIDUM apongezwa na Raisi wa Burundi kushiriki kwenye ufunguzi wa CRDB Bank asubuhi ya leo... - Kora Entertainment
Home » » KIDUM apongezwa na Raisi wa Burundi kushiriki kwenye ufunguzi wa CRDB Bank asubuhi ya leo...

KIDUM apongezwa na Raisi wa Burundi kushiriki kwenye ufunguzi wa CRDB Bank asubuhi ya leo...

Written By Unknown on vendredi 7 décembre 2012 | vendredi, décembre 07, 2012

Kidum kibido akiacha hoyi wageni na pini lake 'Kimbia'


Mwanamuziki wa kimataifa Mrundi Jean Pierre NIMBONA Kidum leo hiyi ameshiriki kama mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa CRDB Bank ambayo makao yake makuu yapatikana nchini Tanzania.Ufunguzi rasmi huyo umefanyika asubuhi ya leo kwenye makao makuu ya bank hiyo jijini Bujumbura.Bank hiyo imejiunga na ingine toka kanda ya East africa inayojulikana kama KCB kutoka Kenya.

Mh Peter Nkurunziza akiwasalimiya baadhi ya Wageni walio kuwepo kwenye ufunguzi rasmi wa CRDB Bank.

Amekuwepo Raisi wa nchi ya Burundi Mh Peter NKURUNZIZA ambaye katika yale aliyo yazungumza ilikuwa nikufurahishwa kwanza na kujijumuisha kwa nchi ya tanzania kuliweka tawi lake la Bank kubwa kama CRDB nchini Burundi,amewasifu kwa jukumu ambalo walilo lichukuwa lakuyaleta Burundi maendeleo.Mtaji wa bank hiyo ni dola biliari 2 sarafu za kimarekeni(2.000.000.000$).

Raisi Peter NKURUNZIZA hakusita vile vile kuwapongeza kwa utendaji kazi wao kwani wamekuja na mfumo mungine kinyume na ingine mifumo inayo tumiwa nchini hapa.Wao sio tu kukaa kwenye ofisi zao bali wanawakuta raia sehemu waliyopo.Kiongozi mkuu wa CRDB nchini hapa Burundi nayeye hakusita kushkuru serekali ya Burundi kwa roho nzuri waliowaonyesha hadi kufurashwa na kushimika mizizi hapa Burundi.Lakufahamu ni kuwa raisi wa nchi ya Burundi alifurashwa sana nakumuona Kidum na hadi kufika kusema:"Ningependa kumshkuru Kidum kuona iko pamoja nasi,unafanya kazi nzuri...".Kwa upande wake KIDUM tulipo mu uliza,alitwambiya:"Ni faraja kubwa kupongezewa na raisi,inanipa picha kubwa ambayo itanifanya nizidishe juhudi ya hali yajuu."Ufunguzi huyo walishuhudiwa vile vile wanao unda kundi la kitamaduni la 'ABAGUMYABANGA',ambalo vile vile lilipata fursa yakurusha watu roho kwa mbwembwe za nyimbo na walivyokuwa wanacheza. 


Baadhi ya picha:
                                                            
    


.

                                                          
Share this article :

0 commentaires:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

Fans Page

Le Béryl Café- Resto- Snack

Visitors

 
Support : Kent-P | Buja News | Kora Entertainment
Copyright © 2013. Kora Entertainment - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website: Kent-P Published by Buja News