CHRIS D:"Burundi ndio nyumbani".(Natimba Bujumbura saa ine usiku Jumaa-tatu). - Kora Entertainment
Home » » CHRIS D:"Burundi ndio nyumbani".(Natimba Bujumbura saa ine usiku Jumaa-tatu).

CHRIS D:"Burundi ndio nyumbani".(Natimba Bujumbura saa ine usiku Jumaa-tatu).

Written By Unknown on samedi 15 décembre 2012 | samedi, décembre 15, 2012

Msanii Mrundi CHRIS D ameshajijengeya sifa kemu kemu kwa upande wa kazi ya muziki anayo ifanya akiwa bondeni(South africa) ifikapo Jumaa-tatu saa ine usiku(22h) atakuwa amewasili nchini Burundi baada ya miaka nenda rudi hakanyagi nchini mwake.Tuliweza kuongeya nae kwa sim na akatufahamisha haya yafwatayo:

Chris d


*AH: Vipi hali yako mwanakwetu?

-Chris d:Hali yangu nzuri sana AH,namshkuru Mungu kuona bado napumuwa kwani kuna binaadamu wamelazwa,wengine mauti uti,ila mimi Mungu bado ananiazima pumzi.

*AH:Kitambo kaka,mbona kimya kirefu?

-Chris d: Hapana wangu,siunajuwa sisi ni watu wa kazi,yaani mishe mishe,kucha kutwa tunajifunza tubuni nini?Tutoke vipi kimistari ili mashabiki wazidi kufaidika kupitiya sisi.

*AH: Mbona hapo kabla ulituahidi utawasili Bujumbura,hadi mda huyu tumekusubiri hadi vizaka vimetuota kwenye roho,kulikoni?

-Chris d: Aaahhhhaaa...acha kunichekesha AH,kweli nimeahidi kipindi kirefu kuwa ntatimba nyumbani ila muda muafaka ulikuwa haujatimiya,ila hivi nalazimika kwasababu kuna issue flani lazima nishuke kwanza nyumbani ili niweze kusafiri kisheria.

*AH: Mpango(issue) gani huyo?

-Chris d:Siunajuwa mimi pamoja na Mh Kidum tutakuwa wabalozi wa Burundi kwenye mashindano ya KORA 2012 yatakayo fanyika nchini Ivory Coast?Sasa inatulazimu tuwe eko,kwani makaratasi tofauti tofauti wameyatuma nchini Burundi ili tuweze kuondokeya nyumbani,na ndio maana imenilazimu nishuke nyumbani.

*AH:Yaani kinyume na mpango huyo hungeweza kushuka?

-Chris d: Burundi ndio nyumbani AH,ningeshuka tu kwani familiya yangu yote iko Burundi."Msahau kwao mtumwa bwana...."


*AH: Utakuwa kama unapita tu!Ao kuna mpangilio mungine kama Show hivo kwani watu kama nyiye muhimu sana,nahuwa hamkosi mialiko ao deal tofati tofauti?


-Chris d: AH,wewe niatari,yaani mpaka ujuwe na chauvunguni?

*AH: Ndio kazi yangu bwana wee...kuelimisha na kukumbusha jamiii...Nambie bana,najuwa washabiki wako Burundi wana kiu chakukuona live ukiwa unawaburudisha kupitiya nyimbo zako,wamechoka nakuziona videos zako,wanaitaji live.

-Chris d:Ni kwweli,tena nafarijika kuskiya hivo.Nilitaka iwe suprise ila ntakundi...ni kwamba niko kwenye mawasiliyano na Big Manager,ni Jamaa flani ambae yuko Burundi,anamapesa yake,tumeongeya sana kuhusu mimi kuifanya Tamasha ila hadi sasa hatuja afikiyana,ila nina imani kuwa tunapo elekeya ni pazuri.

*AH: Msafara kujielekeza Ivory Coast lini?

-Chris d: Itakuwa mbele ya tarehe 29,nakuja kushughulikiya mpango mzima wa safari(makaratasi,tiketi ya ndege na vinginevyo).

*AH:Uko kundi moja na Kidum,Alikibaa(Best male artist in East Africa) huna uoga kweli?

-Chris d: Mimi ni Mwanamuziki,najiamini nakusema niwe katika hivyo vigogo,sikujichagua bali nimechaguliwa kulingana na kazi yangu nzuri,kwa uoga ndo sina sema ni sehemu nyingine ya maisha,najihisi kuwa sasa ndoto yangu inaelekeya pazuri.Atakae shinda ndie atakuwa mwenye bahati kwani "asie kubali kushinda si mshindani",natowa pongezi kwa washabiki wangu wote ambao hadi mdaa huyu wanazidi kunipa shavu kupitiya+22556262626 ,nawaomba wasichoki,nataka akipenda Mungu baada ya Kadjanin iwe mimi,tuiyandike ingine historia kwenye mashindano hayo...

*AH: Tunakutakiya kila la kheri,utaingiya Burundi saa ngapi?

-Chris d:Amin...akipenda Mungu ntatoka Johanesbourg saa tisa na nusu(15h30),kutokana na tiketi nimeikata ntafika Bujumbura saa ine ya usiku(22h).

*AH:Shukran sana,na ujio mwema...

-Chris d: Mimi ndo wakukushkuru AH kwa kazi nzuri unayo tufanyiya sisi Wanamuziki...
Share this article :

0 commentaires:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

Fans Page

Le Béryl Café- Resto- Snack

Visitors

 
Support : Kent-P | Buja News | Kora Entertainment
Copyright © 2013. Kora Entertainment - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website: Kent-P Published by Buja News