Wachezaji wa Burundi na wa kenya waki ingia uwanjani dakika cace kipenge kipulizwe... |
Leo hii kwenye uwanja wa Mwanamfalme Louis rwagasore tumeshughudia pambano la awali lakuwaniya tiketi yakushiriki kwenye fainali za kombe la wachezaji wanaochezea nyumbani maarufu kama CHAN.Burundi nyumbani imejiandikisha ushinde wa bao 1 kwa 0 zidi ya timu ya Harambe Star kutoka Kenya.Bao hilo lilifungwa kwenye dakika ya 28 na kijana NDUWARUGIRA Christophe alias Lucho,anachezeya club ya lydia Ludic.Burundi kipindi cha kwanza ilionyesha kandanda safi,ilizipata na fasi nyingi ila haikuzitumiya ipasavyo.Walipotoka mapumzikoni walizipata walifunga bao mbili ila marefa kutoka Rwanda wakesema kuwa wachezaji walio funga kuwa walioteya na bao hizo kukataliwa,kwa upande mungine kenya ilikuja juu kipindi cha pili ila bahati ndio walikosa.Ngome ya nyuma ya Intamba Murugamba ilisimama vizuri nakulinda vyema lango lao.Dakika 90 zikawa zimemalizika kwa ushindi wa Burundi wa bao 1 kwa 0 ya kenya,marudiyano ni nchini Kenya mu wiki 2.
0 commentaires:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !