Emelance Emy NIWIZERE ameshinda kwenye mashindano ya Sica Awards 2012 nchini Benin..... - Kora Entertainment
Home » » Emelance Emy NIWIZERE ameshinda kwenye mashindano ya Sica Awards 2012 nchini Benin.....

Emelance Emy NIWIZERE ameshinda kwenye mashindano ya Sica Awards 2012 nchini Benin.....

Written By Unknown on dimanche 25 novembre 2012 | dimanche, novembre 25, 2012




Mwanadada Nyota wa mziki nchini hapa Burundi Emelance Emy NIWIZERE mwaka huyu alikuwa balozi wa Burundi kwenye mashindano ya SICA 2012 mashindano yalifanyika nchini Benin,mjini Cotonou ambapo nchi zifikazo 44 zilialikwa kushiriki mashindano hayo,bara la Afrika limewakilishwa na nchi zifwatazo( Afrika ya kusini,Algérie,Bénin(wenyeji),Burkina-Fasso,Burundi,Cameroun,Centrafrique,Congo (Brazzaville),DRC,Côte d'Ivoire,Egypte,Ethiopie,Gabon,Ghana,Guinea bissau,Equatorial Guinee,Guinea Konakry,Lybie,Mali,Maroc,Mauritanie,maroc,Nigeria,Niger,Rwanda,Senegal,Sychelles,sierra leone,Soudan,Tchad,Togo na Tunisia).
 Kwenye mashindano hayo zilialikwa nchi zingine tofauti tofauti kama (Arabie saudite,Koweit,Liban,Palestine,Qatar,Syria,Bahrein,Bresil,Canada,France,Oman  na Irak.)
Mashindano hayo yalikuwa yameingiya kwenye msimo wake wa 8(8e edition) na mwaka huyu mada ikiwa "Maleria,iwe mbali na Africa".Yalianza tarehe 16 November nayakawa yamegonga ukuta hapo jana jumapili jioni tarehe 25 November 2012.Mwaka huyu zimetolewa tunzo 6,na kati ya hizo pako:
*Tunzo ya nyimbo bora inayo ambatana na utamaduni waki africa,unachaguliwa kulinganisha ufundi wake,maneno yake nikimaanisha utunzi mzuri.(Emelance alichukuwa tunzo lenyewe,hongera sana)
*Tunzo ya Presenter live(MC),Burundi mwaka huyu alikuwa amesafiri Edouige MBONIMPA,ila aliambuliya patupu.Video bora
*Tunzo ya Public.
*Tunzo kubwa ya SICA.
*Tunzo la ambae anajituma kwakubadili utamaduni wa Africa.


Msanii wa kike Emelance kutoka Burundi kupitiya nyimbo yake 'Yambogorera' anakuja kuwa wa 2 kujinyakuliya tunzo hilo baada ya Steven SOGO IRAMBONA kulitwa mwaka 2009 kupitiya pini yake 'Il est beau mon pays'.ikumbukwe tu ya kwamba walishiriki waimbaji Albert KULU mwaka 2010,Shazzy Cool HARERA mwaka 2011 wote hao wawili wakawa wameambuliya patupu.Haishangazi sana kwa mwanadada huyo mwaka jana alijanyakuliya tunzo la East African Awards nchini kenya,akashiriki kwenye mashindano ya Couleurs talents kupitiya RFI,Radio ya wafaransa,kote huko alikuwa akizipata heko na saluti za wapenzi wa mziki.Hongera sana Emelance,umerejesha heshma kwa nchi yetu baada ya miaka 3 kutotwa tunzo hilo...














Share this article :

0 commentaires:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

Fans Page

Le Béryl Café- Resto- Snack

Visitors

 
Support : Kent-P | Buja News | Kora Entertainment
Copyright © 2013. Kora Entertainment - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website: Kent-P Published by Buja News