Jana usiku mida ya saa ine dakika 15(22h45)ndipo Mwanamuziki MUGANI Desire a.k.a El burundiano,a.k.a Big farious aliwasili nchini Burundi baada ya msafara mrefu alio ufanya kutokea nchini Ufaransa/Mjini Lille.Farious hapo jana alipokelewa kwa shangwe na jopo la wanao anda mashindano ya Primusc 2012,alipokelewa nwa Watangazaji,na ndugu jamaa na rafiki ambao hawakujali mdaa wa usiku alio fikiya.Kwa upande wa kamati tendaji ya Primusic ni faraja kubwa sana.
Washabiki walio hudhuria na wao pia walionyesha furaha kwakumuona Big ambae walikuwa mara kwa mara wanamuimba nakuitaji kujuwa atatuwa lini nchini Burundi.Big kwa upande wake alifurahi sana kuona kitambo sasa alikuwa haiko nchini,miaka miwili(2ans) sasa kitu ambacho hakusita kusema
Pichani El Maoussen(GLM),Big Fizzo na AH(Burundi News). |
:"Sio siri niikuwa nimepa miss nyumbani,wala nilikuwa sitegemeyi kwamba ningeliweza kurudi mwisho wa mwaka kama hivi,nazitowa pongezi na shukran kwa Washabiki wote waliojitoleya kuja kunipokea aeroport,timu nzima ya Brarudi ambao tulibaki nao kwa mawasiliano mda wote kusema msafara wangu huyu ukamilike na vile vile Watangazaji wote walio nionyesha upendo na mara kwa mara kuniuliza mpangilio mzima wa ujio wangu nchini."Aliongeza nakusema:"Nimekuja kama mchezaji wakulipwa,kweli kila raia anajuwa kuwa nimekuja kwa niaba ya Primusic 2012,hasa kuwashindikiza wadogo zangu kimziki kwenye robo fainali,nusu fainali na hadi fainali,ila kama unavyojuwa AH mimi ni Mwanamuziki myaka 2 sipo nchini nimejifunza na nimeupa muelekeo mziki wa nyumbani kitu ambacho hadi mda huyu kilinifanya niteremke ili namimi nije ku utowa mchango wangu ili tuona kwamba muziki utasonga mbele zaidi.Kuna wadogo wengi wanaweza nafkiri naweza kuwa mwizi wa fadhila endapo sikuwa shavu,yaani nifanye nao collabo kwa wale ntakao wahitaji mimi ama kwa wale watakao nihitaji,ninayo foleni ya ma undegrounds,japokuwa hawataki tuwaite hivo ila nalazimika kwani inabidi watumike vyakutosha ili nawao wafike kwenye level ambayo yumeifkiya sisi kwa sasa.Nimekuja kwenye mpangilio mzima wa Primusic ila hapa kati kati sinto ikaa baana kwani mimi Mchezaji wakulipwa,ninaitaji kutengeneza album yangu mpya kwenye likizo fupi nitakayo ifanya,video vile vile zakushindikiza album yangu lazima nizifanya,nakuja kutumika vyakutosha,alisema kwa lugha ya kifaransa(Je viens bosser dur car 2 ans c'est beaucoup pour un Artiste du Grand renomme comme moi).Nitakapo maliza kuhusu mpango mzima wa Primusic na hayo mautundu flani flani lazima kama niivyo ahidi kitambo ntapita naibuka South Africa ntakuw kule na Mchizi wangu Chris Dizzo ili tuweze kuwakubalisha Washabiki wetu kwenye miji mbali mbali ya kule kama Cap town,Johanesbourg...
Fahamu ya kuwa Big alikuwa aliandaliwa kufikiya Mutanga Nord ila akaomba kuwa ataftiwe Hotel sehemu nyingine,na kamati tendaji hawakusita na alipo lala inakuja kuwa siri kwani anaitaji kupumzika vyakutosha ili ajiandae na msafara wa Kirundo ifikapo kesho asubuhi.
Farious aliwatembeleya Watakao pambana kwenye mashindano ya Primusic 1/4 final... |
Hakusita kuzuru kambi ya Wanamuziki 12 ambao watapambana hapo kesho,aliwapongeza nakuwaomba watumike vyakutosha kwani safari bado ni ndefu inahitaji kujituma na kuwa na roho ya subira.Kidum Kibido,Big Farious na Mkomboz ndio watakuwa wageni rasmi kesho Mkoani Kirundo ili waweze kuelimisha,kuburudisha Washabiki wa burundi flava.
Hizi ni baadhi ya picha tulizo zichukuwa pale...
Apo alikuwa anatoka... |
Sat b na Mkeo walikuwa kati ya walio wasili uwanja wa ndege kuja kumpokea Big fizzo. |
Farious na Raymond,ilikuwa ni furaha kuonana ana kwa ana kwani Raymond ndie alijiusisha na mpangilio wakumkatiya tiketi akiwa nchini Ufaransa. |
Ilikuwa ni faraja isio kuwa na mfano kwa Sat b kumpokea The general... |
vizuri
RépondreSupprimer