Big Farious:"Msahau kwao mtumwa.."(Bujumbura jumaa tatu hii saa moja usiku) - Kora Entertainment
Home » » Big Farious:"Msahau kwao mtumwa.."(Bujumbura jumaa tatu hii saa moja usiku)

Big Farious:"Msahau kwao mtumwa.."(Bujumbura jumaa tatu hii saa moja usiku)

Written By Unknown on lundi 26 novembre 2012 | lundi, novembre 26, 2012


El Burundiano

'Lisemwalo lipo na kama halipo basi lipo njiani'.Naanza na mesali hiyi ya kiswahili ili kukupa wewe raia wa Burundi ambae pengine waweza kuwa na hofu ya kutowasili nchini kwa MUGANI Desire a.k.a El Burundiano.Ameshajijengeya sifa  nje na ndani ya Burundi kwa kazi nzuri anayo ifanya ya muziki,alikuwa anakula zake kuku kwa mkenge nchini Ufaransa ila ameamuwa kurejeya nchini kama alivyotufahamisha:"Msahau kwao mtumwa".Tulipo hojiana naye kwa sim akiwa mjini Lille/Ufaransa alitwambiya haya machache:

AH:Habari yako?
Big Farious:Niko poa sana bro.
AH:Kunafununu zinasema kuwa utateremka nyumbani Jumaa tatu,ao ni uzushi?
Big Farious: La hasha!Sio uzushi mbona habari zote huwa mnasema ni uzushi?Mimi nateremka jumaa tatu.
AH:Kulikoni?
Big Farious:Siunajuwa kitambo siji home,niliahidi sana,ila mda wenyewe ndio huyu.
AH:Tumeskiya umesaini mkataba na Brarudi kuhusu swali nzima la Primusic 2012?
Big Farious:Hiyo haina kasoro,ningelipongeza kwanza kamati nzima kwani mpangilio wao nomaa....
AH:Yani umefurahishwa na mashindano yenyewe?
Big Farious:Ningelikuwa Waziri ao najiusisha na swali nzima lakutowa Awards basi bila shaka wangeipata mwaka huyu,kwani ilikuwa haijatokeya,hongera saaana...
AH:Mipangilio yako ni ipi nchini kwa likizo utakayo ichukuwa?
Big Farious:Aaahhh...sijafika bwana,acha nikifika ntawafahamisheni.Ila nakufahamu narejeya nchini kwa niaba ya Primusic,ila tamasha na mengi tu kama kuzirikodi pini nyimpya iyo haina mushkil...
AH:Utafika sangapi?
Big Farious:Akipenda mungu,saa moja usiku na ndege aina ya Brussels airlines...
AH:Una ahidi nini warundi na wapenzi wako,nikimaanisha washabiki wako?
Big Farious:Nakuja nchini tuambukizane furaha,tuchangiye,tushahuriane,tukosowane palipo makosa,tuongozane kupitiya mziki ili tusake kwa pamoja njia mbadala ya maendeleo  kwa ujumla nchini kwetu
AH:Twakutakiya kila la kheri na fanaka,ujio mwema...
Big Farious:Shukran sana na pongezi kwa kazi yako...
Share this article :

1 commentaire:

Commentaire

Fans Page

Le Béryl Café- Resto- Snack

Visitors

 
Support : Kent-P | Buja News | Kora Entertainment
Copyright © 2013. Kora Entertainment - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website: Kent-P Published by Buja News